Ruto kuhudhuria mdahalo wa wagombea urais tarehe 26 Julai

Mrengo wa Naibu wa Rais William Ruto umetoa taarifa kuhusu namna mdahalo wa wagombea wenza wa urais ulivyofanyika wiki hii.

Kupitia taarifa, Mkurugenzi wa Mawasiliano katika kampeni za Ruto Hussein Mohamed amesema kuwa mrengo wao umebainisha kuwa mdahalo huo haikuifanya kipaumbele matakwa ya umma.

Badala yake, Hussein amesema kuwa muda mwingi ulitumiwa na waendesha mdahalo wenye kuangazia masuala binafsi.