Waiguru atakiwa kusalia kimya kuhusu sakata ya NYS


Na Mate Tongola
NAIROBI, KENYA, Aliyekuwa Waziri wa Ugatuzi, Ann Waiguru ametakiwa kutotoa matamshi yoyote kuhusu sakata ya ufujaji wa kima cha shilingi bilioni 1.6 katika Taasisi ya Kitaifa ya Huduma za Vijana, NYS.

Uamuzi huo umetolewa na Hakimu Mkuu wa mahakama ya Nairobi David Mburu kufuatia ombi la lililowasilishwa na mmoja wa washukiwa wa sakata hiyo, Paul Kinuthia Kihara ambaye alidai kwamba Waiguru ambaye ametangaza nia ya kuwania ugavana kwenye Kaunti ya Kirinyaghah analitumia suala hilo kujitafutia umaarufu wa kisiasa.
Washukiwa tarkiban 11 wanahusishwa na ufujaji wa fedha za NYS wakati Waiguru alipokuwa Waziri wa Ugatuzi.

 

Related Topics

Waiguru NYS