Raila Asema Sheria za Matiang'i Zimefeli

Na, Beatrice Maganga

Sheria mpya za elimu zilizobuniwa na Waziri Fred Matiang'i zimefeli. Ndiyo kauli ya Kinara wa CORD Raila Odinga ambaye amesema huenda visa vya moto shuleni vinachochewa na sheria hizo.
Kwenye taarifa kwa vyombo vya habari akiwa kwenye jimbo la Philadelphia Marekani, Raila  ameikosoa sheria kwamba wanafunzi wasio watahiniwa wasalie nyumbani wakati wa mitihani ya taifa, akisema hatua hiyo si suluhu ya udanganyifu kwenye mitihani hiyo. Aidha amekosoa hatua ya Matiang'i kupiga marufuku maombi muhula wa tatu na suala la wanafunzi kutembelewa na wazazi wao muhula huo.
Ameitaka serikali kudhibiti udanyanyifu wa mitihani kuanzia Baraza la Mitihani nchini KNEC ambalo hutunga mithani hiyo badala ya kuwalazimishia wanafunzi sheria zisizo na msingi.
Wakati uo huo ameitaka serikali kuwahakikisha wanafunzi usalama wao ikizingatiwa kwamba visa vya moto shuleni vinaendelea kuripotiwa kila kukicha.

 

Related Topics