Pep Guardiola Hana "Bifu" na Morinho!

Na, Stephen Mukangai

MENEJA wa Manchester City Pep Guardiola amesema kuwa hana tatizo na kumsalimu kwa mkono mwenzako wa Manchester United Jose Mourinho.

Akiwajibu wanahabari waliotaka kujua iwapo bado ana roho ngumu dhidi ya Mourinho, Guardiola amesema kuwa alimsamehe Mourinho na yuko tayari kufanya kazi naye katika ligi ya premier. "Namheshimu Mourinho kama kocha mwenzangu na tutakapo kutana nitamsalimu kwa mkono" Alisema.

"Tulikuwa sote katika timu ya Barcelona kwa kipindi cha miaka mitano na tulijifunza mengi pamoja kwa muda huo," Aliendelea.

Kwa upande wake alipoulizwa Mourinho alisema kuwa atamsalimu Guardiola kwa mkono.

MOURINHO na Guardiola walikuwa na uhasama mkubwa walipokuwa katika ligi ya La Liga nchini Uhispania na Jumatatu, Julai 25 watakutana wakati wa mechi ya kirafiki kati ya Manchester United na Manchester City mjini Shanghai Uchina.