Grenade found at PMs Office - Swahili

Maafisa wa polisi waliimarisha ulinzi wao ndani na nje ya afisi za waziri mkuu baada ya aina ya guruneti kupatikana nje ya afisi ya waziri mkuu mapema hii leo na kuzua hali ya taharuki. Maafisa wa polisi wakiwemo wale wa kudhibiti mikasa walifika kwenye eneo hilo kwa haraka na kufanya uchunguzi wao. Hata hivyo naibu msemaji wa polisi Charles Owino alieleza kuwa uchunguzi ungali unaendelea kubaini ni nani aliyeweka guruneti hilo na nia yake ilikuwa gani.