Kibaki Apinga Ufisadi

Rais Mwai Kibaki hii leo ametoa matamshi makali akiwashutumu maafisa wakuu serikalini ambao ni wafisadi. Rais amesema wakenya hawafai kabisa kuwaonea huruma waliohusika na ufisadi. Kibaki aliyasema haya huku mawaziri wake watano wakihusishwa na tuhuma za ufisadi katika wizara mbali mbali.