Jukumu la mwalimu haswa ni nini, ni swala ambalo linahitaji ufafanuzi tena katika taswira ya visa vya walimu kuwabaka wanafunzi. katika miaka ya awali kando na jukumu kuu la mwalimu kuwa ni lile la kuwafunza watoto, mwalimu alikuwa mlezi na mwenye kuwapa mwongozo mwema watoto wa shule. ilitubidi kumtafuta mwalimu mwenye uzoefu mkubwa wa kufunza kutufahamisha tena jukumu kamili la mwalimu.