Aliyekuwa Askofu Mkuu wa Kanisa Katoliki Raphael Ndingi Mwana 'a Nzeki amefariki dunia.
a'Nzeki ameaga dunia akiwa na umri wa miaka themanini na minane baada ya kuugua kwa muda mrefu. Taarifa ya kifo chake imetangazwa na Askofu Mkuu wa Kanisa Katoliki John Njue, ambaye amewashauri waumini na Wakenya kuiombea familia ya Ndingi kipindi hiki kigumu.