Hayati Mzee Daniel Toroitich Arap Moi ametajwa kuwa Kigogo wa Kisiasa, nguzo kuu ya maendeleo, amani na ushirikiano baina ya Kenya na mataifa ya Jumuiya ya Afrika.
Marais wa mataifa zaidi ya matano ya Afrika wamesema kuwa Mzee Moi alichangia pakubwa kuimarika kwa miungano ya maendeleo ya Bara la Afrika yakiwamo EAC, IGAD na COMESA.
Wakizungumza wakati wa Ibada ya Kitaifa ya Mzee Moi katika Uwanja wa Nyayo hapa jijini Nairobi, marais hao wakiongozwa na Yoweri Museveni wa Uganda wamemmiminia sifa tele Hayati Moi wakimtaja kuwa kiongozi aliyeleta amani nchini na kwenye mataifa ya Afrika.