SECTIONS

Palos Kileleni mwa NSL

Na Andrew Shonko
Viongozi wa ligi ya divisheni ya pili NSL Palos FC waliwapiku vijana na wa Frank Ouma Wazito FC 2-1 katika mechi iliyoandaliwa uwanjani Camp Toyoyo Ijumapili. 
Bao la Morven Otinya katika kipindi cha kwanza kiliihakikishia Palos ushindi na kuwaacha wakiwa uongozini mwa Jedwali la NSL na alama saba. GFE 105 ni wapili na alama sita nao Ushuru FC wanafunga tatu bora wakiwa na usawa wa alama na GFE. 
Kibera Black Stars na Nairobi City Stars bado hawajaandikisha ushindi wowote ambao unaawacha wakiwa wa mwisho.
Matokeo
wazito Fc 1-2 palos Fc 
Agrochemicals 0-0 Fc Talanta 
kibera black stars 1-2 Police Fc
 Nairobi stima 2-1 Bidco united 
Isibania 0-2 Ushuru FC