Maafisa wa utoza ushuru KRA wamenasa shehena nyingine ya pembe za Ndovu katika bandari ya Mombasa . Pembe hizo mia saba ishirini na tano ni moja wapo ya shehena kubwa zaidi kupatikana na pembe za ndovu. Hii ni mara ya pili mwezi huu kupatikana kwa shehena kama hiyo . Idara ya usimamizi wa wanyama pori- kws inasema kizingiti kikubwa cha kukabiliana na biashara haramu ya pembe za ndovu ni uhafifu wa sheria iliopoa ambapo watuhumiwa wanapotiwa mbaroni hupewa faini ya kati ya shilingi elfu 2 hadi 30, ambazo wana uwezo wa kuzilipa- au kifungo cha miezi sita. KWS inasema afueni ni kupitishwa kwa mswaada wa wanayma pori unaotoa sheria kali kwa watuhumiwa.