KRA: Q2 Results

Mamlaka ya utozaji ushuru nchini, KRA imetangaza kuwa imepita malengo yake ya utozaji ushuru katika kipindi cha miezi mitatu iliyopita. Shirika hilo lilisema liliweza kukusanya shilingi bilioni mia moja na thelathini na nne katika kipindi hicho. Vilevile KRA ina matumaini makuu kuwa itaweza kupita malengo ya ukusanyaji ushuru mwaka huu.