JUBILEE CHATOA VYETI ZAIDI HUKU WALIONYIMWA WAKILALAMIKA

Na Sophia Chinyezi

Chama cha Jubilee leo kimeendeleza shughuli ya kuwakabidhi vyeti washindi wa uteuzi wa chama hicho katika maeneo mbalimbali nchini. Katika Kaunti ya Mombasa Shughuli hiyo ilikumbwa na utata baada ya chama hicho kukataa kutoa cheti kwa muwaniaji wa ubunge Nyali. Wawaniaji wa Kiti hicho Mohamed Salim maarufu Tenge na Omar Shallo, wote walitaka kukabidhiwa cheti, ingawa tangazo lilitolewa kwamba kulikuwapo na hitilafu, hivyo cheti hicho hakingeweza kutolewa.

Hata hivyo Suleiman Shahbal amekabidhiwa cheti kuwani Ugavana, huku Kassim Abulsalam akpokezwa cheti kuwania wadhifa wa useneta, baada ya kumshinda Naibu Gavana wa kaunti hiyo Hazel Katana. Karisa Nzai atawani Ubunge. Akizungumza baada ya kupewa cheti chake Nzai amewaomba walioshindwa kuungana na wenzao ili kuiendeleza kaunti hiyo.


Wengine waliokabidhiwa vyeti vyao ni Daib Ali, Amina Abdalla, Ashraf Bayusuf, Francis Lewa na Masoud Mwahima. Mshirikishi wa Chama cha Jubilee Nairobi, Susan Maina aliongoza shughuli hiyo katika Kaunti ya Machakos. Akizungumza katika hafla iyo hiyo Mshirikishi wa chama hicho eneo la Machakos Jeremiah Kamia, Chama cha Jubilee kina imani kuwa kitapata uungwaji mkono wa idadi kubwa ya wenyeji wa  kwa wingi katika kaunti ya machakos.


Aidha mwanasiasa anayewania ubunge wa Mwala Joseph Nzeki amewarai wakazi wa Machakos kuwachagua viongozi kwa kuzingatia sera zao wala sio chama.

Related Topics