Mt. Elgon - Wajane wadai fidia 9/04/09

 

Viongozi wa madhehebu kutoka eneo la Mount Elgon wanaitaka serikali ya Kenya kuwalipa fidia wanawake elfu moja mia mbili ambao kufikia sasa ni wajane baada ya waume wao kufariki katika makabiliano ya vita kuhusu ardhi kwenye eneo hilo . Hii ni baada ya operesheni iliyoanzishwa na serikali ya kuwasaka wanachama wa kikundi cha kigaidi cha Sabaot Land Defence Force.