Mtu mmoja ameaga dunia na wengine kadhaa kujeruhiwa vibaya kwenye ajali ya barabarani, iliyohusisha magari 4 katika Nairobi Expressway, usiku wa kuamkia Jumapili.
Kwenye ajali hiyo ya kwanza kabisa katika Nairobi Expressway, dereva mmoja alikuwa akiendesha gari lake kwa mwendo wa kasi zaidi, hadi akashindwa kudhibiti usukani na kugonga magari mengine matatu yaliyokuwa yakisubiri kupewa idhini ya kuondoka kwenye Barabara ya Nairobi Expressway, baada ya kulipa ada za kutumia barabara hiyo.