Kwenye podikasti ya Kulikoni leo, ninaongea naye Daktari Jonathan Choti wa chuo kikuu cha jimbu la Michigan (Michigan State University). Yeye ni muhadhiri nguli wa maswala ya lugha za Kiafrika. Pia ni mwanachama wa kikundi cha wasomi wa kutoka Kenya yaani Kenya Scholars and Studies Association (KESSA). Mada yetu ni hali halisia ya ukufunzi wa lugha za kiafrika Marekani, hususan Kiswahili. Karibuni nyote!