Mswada wa Fedha 2024/2025: Je, Kenya Kwanza Inakujali Wewe?
Published May. 17, 2024
00:00
00:00

Mapendekezo yaliyomo kwenye Mswada wa Fedha wa mwaka wa kifedha ujao yanaonesha wazi kuwa serikali ya Kenya Kwanza haina ufahamu wa hali halisi ya Mkenya. Haijali kuhusu vipaumbele vya Mkenya. Lakini, nani aliiweka serikali hii mamlakani kama sio Mkenya yuyu huyu. Huwa tunauliza maswali kuhusu nani atafadhili ahadi chungu nzima zinazotolewa na wanasiasa wakati wa kampeini?