Kifo cha CDF Ogolla Kimezua Maswali Mengi; Wakenya Wadai Majibu
Published Apr. 22, 2024
00:00
00:00

Kweli ajali haina kinga. Hata hivyo tukio la Jenerali wa Jeshi la Nchi kufariki kwenye ajali ya ndege, akiwa ndani mwa nchi yake, ni jambo ambalo lazima lichunguzwe. Je, kunao waliolala kazini kiasi cha kuruhusu tukio hili kutokea au ni ajali tu kama ajali nyingine? Lazima pafanyike uchunguzi wa kina kubaini kilichojiri.