Je, Nairobi Iko Tayari Kukabiliana na Mvua Kubwa?
Published Mar. 26, 2024
00:00
00:00

Mvua iliyonyesha usiku wa Jumapili imesababisha mauti na uharibifu mkubwa jijini Nairobi. Mvua hiyo imeonesha wazi jinsi miundomsingi iliyopo haina uwezo wa kustahimili mvua kubwa, hivyo kuna haja ya uekezaji wa kumaanisha katika miundomsingi ya ukusanyaji maji taka (drainage) ili kuwaepushia wakazi madhara.