Kenya Kusaidia Haiti- Je, Ni Kafara au Ushujaa?: Sepetuko
Published Mar. 11, 2024
00:00
00:00

Marekani imeanza kuwaondoa nchini Haiti raia wake wanaofanya kazi kwenye Ubalozi wake nchini humo. Wakati uo huo, serikali ya nchi inaiomba Kenya kuharakisha mchakato wa kuwatuma maafisa wake wa polisi kuenda kudumisha usalama katika taifa hilo la eneo la Karibea. Hayo yanajiri huku magenge ya uhalifu yakiendeleza uhalifu katika nchi hiyo ya jumla ya watu milioni 11. Sepetuko inakariri kuwa kuwatuma maafisa wa polisi katika taifa hilo ni kuwatoa kafara wana wetu. Mbona serikali isifanye kipaumbele usalama wa raia wake kuliko kuwatuma walindausalama zaidi ya kilomita elfu 12 kutoka Kenya?