Miaka 30 ya Kusubiri-Mwanajeshi Mstaafu Ahangaika Kupata Pensheni
Published Mar. 07, 2024
00:00
00:00

Isaiah Ochanda, Afisa wa Jeshi aliyestaafu alifika mbele ya Kamati ya Ulinzi ya Seneti akiwa kwenye kitanda cha hospitalini. Ochanda alistaafu kutoka Jeshini miaka ya 1990s na kwa miaka hiyo yote juhudi zake za kupata pesa zake za baada ya kustaafu zimegonga mwamba. Kulikoni? Mbona wafanyakazi wa serikali waliostaafu hutaabishwa mno kupata malipo ya uzeeni? Iko wapi serikali kuangazia suala hili?