×
App Icon
The Standard e-Paper
Truth Without Fear
★★★★ - on Play Store
Download Now

IEBC yatoa tahadhari kwa wanasiasa wanao vuruga chaguzi

Mwenye kiti wa tume ya IEBC Erustus Ethekon akipokea karatasi za kupiga kura katiak uwanja ndege wa JKIA. [Collins Oduor, Standard]

Tume Huru ya Uchaguzi na Mipaka (IEBC) imetoa onyo kali kwa wanasiasa wanaodaiwa kuwatisha na kuingilia majukumu ya maafisa wa uchaguzi, ikisema vitendo hivyo vinahatarisha uadilifu wa chaguzi nchini.

Mwenyekiti Erastus Ethekon, amesema kuwa tume hiyo imebaini mwenendo hatari katika chaguzi ndogo za hivi majuzi, ukiwemo pamoja na wanasiasa kujitambulisha kama ‘mawakala wakuu’ kuvamia vituo na kuingilia taratibu za uchaguzi.

“Hawa wanaoitwa mawakala wakuu hawana mamlaka ya kuvamia vituo na kuanzisha mchakato wao. Hatutalikubali kamwe,” Ethekon alisema wakati wa kikao cha tathmini ya chaguzi ndogo za Novemba 27 jijini Nairobi.

Aliongeza kuwa yeyote atakayevuruga utaratibu wa uchaguzi au kuwadhulumu maafisa wa tume atachukuliwa hatua kali za kisheria.


SOMA: IEBC warns political actors against trying to influence election officials

“Kumtisha au kumshambulia afisa wa IEBC si siasa, ni kosa la jinai na watakaohusika lazima wawajibike,” Ethekon alisema.

Matamshi yake yanakuja baada ya tume hiyo kukosolewa kwa kuchelewa kuchukua hatua dhidi ya visa vya vurugu vilivyoripotiwa katika maeneo ya Mbeere Kaskazini, Malava, Kasipul, na baadhi ya wadi za Nyamira, Machakos na Nairobi.

Pia kuliripotiwa madai ya ununuzi wa kura na ugawaji wa chakula cha msaada kabla ya uchaguzi, hatua iliyodaiwa kuwapotosha wapiga kura.

Licha ya changamoto hizo, IEBC ilisema mfumo wa KIEMS ulifanya kazi ipasavyo katika vituo vingi, na upigaji kura uliendelea bila changamoto za kiufundi.

Ethekon aliwaonya wanasiasa kuwa kuendelea kuvuruga shughuli za uchaguzi kunaweza kuhatarisha uaminifu wa Uchaguzi Mkuu wa 2027.

“Uchaguzi ni mali ya wananchi, sisi ni wasimamizi wa mchakato huo, si wanasiasa,” alisema.