×
App Icon
The Standard e-Paper
Home To Bold Columnists
★★★★ - on Play Store
Download App

Abraham Serem Ateuliwa kuwa Kaimu Afisa Mkuu Mtendaji wa KenGen

Abraham Serem ndiye Kaimu Afisa Mkuu Mtendaji wa Kampuni ya KenGen baada ya kuteuliwa kushikilia wadhifa huo. Serem anachukua nafasi hiyo kutoka kwa Rebecca Miano ambaye ameteuliwa kuwa Waziri wa Jumuiya ya Afrika Mashariki, Maeneo Kame na Maendeleo katika Maeneo.

Katika notisi iliyochapishwa na Mwenyekiti wa Bodi ya Kengen, Samson Mwathethe kwenye magazeti ya humu nchini leo hii, imesema kwamba Serem atahudumu katika wadhifa huo hadi wakati mtu mwingine atakapoteuliwa kwa wadhifa huo.

Serem amekuwa akihudumu katika wadhifa wa Meneja Mkuu vilevile mkuu wa wafanyakazi tangu Machi mwaka 2016. Ana tajriba ya miaka 20 katika kitengo cha kuwahudumia wafanyakazi, HR.

Get Full Access for Ksh299/Week
Bold Reporting Takes Time, Courage and Investment. Stand With Us.
  • Unlimited access to all premium content
  • Uninterrupted ad-free browsing experience
  • Mobile-optimized reading experience
  • Weekly Newsletters
  • MPesa, Airtel Money and Cards accepted
Already a subscriber? Log in