Aliyekuwa Gavana wa Nairobi Mike Sonko amejitolea kwa mara nyingine kumsaidia aliyekuwa mwanandondi Conjestina Achieng, baada ya picha ya Conjestina maarufu Conje, kusambaa mitandaoni na kuibua hisia za kuhuzunisha.
Katika Mtandao wa Twitter, Sonko amesema tayari ametuma gari moja hadi nyumbani kwa Conjestina ili kumsafirisha hadi Mombasa kwa ajili ya maombi.