Sheria ya kuwapiga teke magavana

Cheo na mamlaka yamekuwa ngao ya kudumu kwa viongozi wa kisiasa kujikinga dhidi ya kashfa za u? sadi huku viongozi wengi wanaotiwa nguvuni wakiachiliwa punde tu baada ya ku? kishwa mahakamani na kutozwa faini au kuachiliwa kwa dhamana.

Mara nyingi kesi huyumbayumba hadi kutupiliwa mbali. Ukosefu wa ushahidi na mashahidi kukosa ku? ka mahakamani kutoa ushahidi wao mbele ya hakimu ni jambo la kawaida kila kuchao.

Jambo hili limewafanya wakenya wengi kupoteza matumaini ya kupata haki mahakamani kwa kesi zinazowahusisha viongozi wa ngazi za juu serikalini na katika ngazi ya Kaunti.

Imani ya Wakenya

Hata hivyo mabadiliko yaliyofanyiwa Tume ya Kupambana na U?sadi nchini na kitengo cha Jinai kinachoshughulikia maswala ya u? sadi vimeinua pakubwa imani ya wakenya na ari yao ya kusaka haki.

Hata hivyo kuimarishwa kwa taasisi hizo imekuwa tisho kubwa kwa uongozi wa Magavana kwani hadi sasa Magavana ambao hawajawajibika kikamilifu katika serikali zao wana kila sababu ya kuwa na wasi wasi kwani endapo kutakuwapo ushahidi wa kuyapa nguvu madai ya matumizi mabaya ya mamlaka watatakiwa kuondoka mamlakani na kusubiri kujua hatima yao nje ya a? si zao.

Gavana Ferdinand Waititu wa kaunti ya Kiambu ndiye wa hivi punde kuvuliwa mamlaka yake na kusalia tu kusubiria matokeo ya kesi ya u? sadi dhidi yake, Waititu anakabiliwa na mahstaka ya kupotea kwa zaidi ya shilingi milioni 500 kutokana na utoaji wa kandarasi bila kuzingatia vigezo muhimu na sheria za utoaji zabuni.

Kinyume na ilivyotarajiwa mahakama imemtaka kusalia nje ya majukumu yake na a? si na badala yake kumkabidhi usukani naibu wake bwana Daktari James Nyoro.

Sheria yazua hofu

Hofu ya Magavana ipo kwenye uhusiano uliodorora kati ya manaibu wao, wabunge na Mawaziri wa kaunti kutumiwa na wapinzani wao kuwasambaratisha kisiasa hasa baada kubainika wazi kuwa maa? sa wakuu serikalini hawatokubaliwa kuendelea kuhudu kulingana na Jaji wa mahakama kuu Bi. Ngene Macharia.

Ni kejeli kisheria kuruhusu mtuhumiwa wa kesi ya u? sadi kuendelea kuhudumu katika a? si ya serikali licha ya kuwa hajapatikana na hatia. Msimamo ulioungwa mkono na mkurugenzi mkuu wa mashtaka umma DPP Bwana Nurdin Haji.

“Kwetu sisi, mwelekeo wetu kutokea mwanzo umekuwa jinsi Hakimu Mumbi Ngugi ameifasiri. Nafahamu kwamba Baraza la Magavana limetenga hela na watawatumia watu wengi kutukabili. Hatuna la kufadhaikia. Tuko tayari kuutetea msimamo wetu, Ni jukumu la mahakama kuifasiri sheria,” amesema Haji.

Magavana wengine wenye kesi za u? sadi dhidi yao ni pamoja na Gavana wa Samburu Bwana Moses Kasaine Lenolkulal ambaye sawa na mwenzake wa Kiambu amezuiliwa kuendelea kutekeleza majukumu yake hadi kesi dhidi yake kusikilizwa na kuamuliwa.

Wakosa usingizi

Hatua ya mahakama kutoa agizo la kuzuiliwa kwa wawili hawa na mkurugenzi mkuu wa mashtaka ya umma Bwana Nurdin Haji kutaka kesi ndhidi ya Gavana wa Busia Bwana Sospeter Odeke Ojamong kutadhminiwa upya na kuamuliwa kama anastahili kuwa A? sini huku kesi yake kuhusu ubadhirifu wa fedha.

Gavana wa kaunti ya Migori Okoth Obado yuko nje kwa dhamana, Obado anatuhumiwa kumuua mwanafunzi wa Chuo Kikuu cha Rongo, Sharon Otieno na mwanawe pamoja na kumiliki silaha bila kibali.

Katika Kaunti ya Garisa hali ni tete, Gavana Ali Korane anachunguzwa na maa? sa wa kitengo cha ujasusi kwa tuhuma za u? sadi. Aidha Inaari? wa kuwa maa? sa wa tume ya kupambana u? sadi nchini EACC wamepiga kambi katika a? si kuu za kaunti mjini Homa bay ambapo Gavana Cyprian Awiti anatuhumiwa kwa ubadhirifu na utoaji wa kandarasi kwa njia isiyofaa.

Magavana na kaunti zinginezo zinazopigwa Kurunzi na tume ya u? sadi - EACC ni pamoja na Mohamed Ali wa Marsabit, Muthomi Njuki wa Tharaka Nithi, Mwangi wa Iria wa Murang’a, Charity Ngilu wa Kitui na Granton Samboja wa Taita Taveta Mwenyekiti wa Baraza la Magavana aliye pia Gavana wa Kakamega Wycliffe Oparanya amewahimiza wanasheria barazani humo kuchunguza iwapo ipo nafasi ya kisheria na kwa kuzingatia haki za kibinadamu kuwaruhusu mgavana wenzake kusalia mamlakani wanapoendelea kujibu mashtaka ya uhalifu wa kiuchumi dhidi yao.

Ijapo siyo manaibu wa magava wote wanaosherehekea sharia hii mpya ya kuwapiga teke miongoni mwa magavana watakaobanwa na kesi za u? sadi, lakini ukweli ni kwamba wengi wao wanasubiri nyundo hiyo kuwaagnukia mabosi wao, ikiwezekana haraka iwezekanavyo.

Siyo kwa kubanduliwa kwa wakubwa wao mao? sini ndio wanyakuwe wadhifa wa bwerere bali wanatamani Mungu naye awaite mapema watangulie mbele za haki ili wapitie katikati kuupata uongozi wa kaunti.

Hali hii imewafanya manaibu gavana kuwa maadui wa ndani kwa ndani na magavana wao ambao Imani dhidi yao imelegea. Ingawa hivyo, lolote linaweza kutokea na wakati huo huo naibu akawa gavana. Jambo hili lawahuzunisha magavana wengi mno.