×
App Icon
The Standard e-Paper
Home To Bold Columnists
★★★★ - on Play Store
Download App

Rais Kenyatta atakiwa kuwateua wanawake

Na, Beatrice Maganga
Rais Kenyatta atakiwa kuwateua wanawake
Huku Rais Uhuru Kenyatta akisubiriwa kulitangaza baraza zima mawaziri, kundi la wanaharakati limewasilisha waraka kwa ofisi ya Rais likimsihi awateue wanawake tisa kuhudumu katika baraza hilo ili kutimiza hitaji la uwakilishi wa kijinsia.
Kulingana na Afisa Mkuu Mtendaji wa mojawapo la makundi ya kutetea haki la Centre for Rights, Education and Awareness, Wangeci Wachira, Rais Kenyatta anastahili kuhakikisha kipengele cha katiba kuhusu usawa wa kijinsia kinatekelezwa kwa ukamilifu. Wachira ameliongoza kundi la wanawake hadi Jumba la Harambee jijini Nairobi kuwasilisha waraka huo kwa Rais.
Wanaharakati hao wanasema wako tayari kupendekeza orodha ya wanawake wanaostahili kuteuliwa kuwa mawaziri. Kufikia sasa, Rais Kenyatta amewataja mawaziri 9 wote wakiwa ni wa kiume.
Get Full Access for Ksh299/Week.
Uncover the stories others won’t tell. Subscribe now for exclusive access
  • Unlimited access to all premium content
  • Uninterrupted ad-free browsing experience
  • Mobile-optimized reading experience
  • Weekly Newsletters
  • MPesa, Airtel Money and Cards accepted
Already a subscriber? Log in

Related Topics