JOHO AKAMATWA

JOHO AKAMATWA
Fredrick Muitiriri
Vita vya ubabe kwenye Kaunti ya Mombasa baina ya Gavana, Ali Hassan Joho na Kamishna wa kaunti hiyo, Nelson Marwa vinaendelea kuchacha. Mapema leo Joho amemsuta Marwa kwa kuwatuma maafisa wa polisi kuwakamata maafisa wa kaunti hiyo waliokuwa wametumwa kubomoa ukuta ambao unasemekana utajengwa katika ardhi ya serikali. Joho ambaye amefika katika kituo cha polisi cha Nyali ambako maafisa hao saba walizuiliwa amesema hataondoka hadi waachiliwe huru. Katika kikao na wanahabari, Gavana huyo ambaye awali alidaiwa kukamatwa, amesema imekuwa vigumu kwa serikali yake kufanya kazi na serikali ya kitaifa na kuongeza kwa atafika mahakamani ili kupata mwanga kuhusu majukumu ya kaunti na ya serikali hiyo ya kitaifa.
Joho amedai kuwa mwaka jana walipata barua kutoka Tume ya Ardhi, NLC iliyoagiza kuwa kipande hicho ni cha serikali na leo hii waliwatuma maafisa wake kubomoa ukuta uliokuwa ukijengwa kabla ya kufumaniwa na maafisa wa polisi na kuwakamata.
Kwa zaidi ya miaka minne sasa, Joho na Marwa wamekuwa wakizozana na kujipiga vifua wakisema wana mamlaka sawa ya kuendesha kaunti hiyo ambayo ni kitovu cha utalii nchini, mbali na kuwa na bandari ya kipekee humu nchini.

Related Topics