Please enable JavaScript to view advertisements.
×
App Icon
The Standard e-Paper
Smart Minds Choose Us
★★★★ - on Play Store
Download App

IEBC yasema haitaifanyia marekebisho sajili ya wapigakura


IEBC yasema haitaifanyia marekebisho sajili ya wapigakura: Carren Omae
''Hatutaifanyia tena marekebisho sajili ya wapigakura.''Ndio msimamo wa Tume ya Uchaguzi IEBC kufuatia malalamishi ambayo yamekuwa yakiibuliwa hasa na upinzani kwamba sajili hiyo ina dosari. Mwenyekiti wa IEBC Wafula Chebukati, amesema wanahitaji muda wa kutosha kwa maandalizi ya uchaguzi mkuu, na kuanza upya shughuli ya kuifanyia marekebisho yoyote sajili vilevile orodha ya wagombea wa nyadhfa za kisiasa, kunaweza kuathiri pakubwa uchaguzi mkuu wa Agosti nane.
Chebukati amesisitiza kuwa sajili iliyofanyiwa ukaguzi na kampuni ya KPMG, ndiyo itakayotumika wakati wa uchaguzi mkuu ujao, kwani masuala yote yakiwamo malalamiko yaliyoibuliwa na wananchi wakati wa muda wa kuthibitisha rekodi zao yalishughulikiwa.
Kuhusu maajeti wa vyama watakaosimamia shughuli hiyo, Chebukati amesema vyama vya kisiasa vinaruhusiwa kumtuma ajeti mmoja pekee katika kila kituo cha kupigia kura, na iwapo hakitafanya hivyo wagombea nyadhifa mbalimbali wanaruhusiwa kuwatuma maajeti wao.
Ikumbukwe NASA ilikuwa imesema kuwa mbali na maajenti itawatuma waangalizi watano katika kila kituo cha kupigia  kura kuhakikisha hakuna kura zitakazoibwa.
Hayo yanajiri huku Muungano wa NASA ukipendekeza bunge kuitisha kikao maalum kijadili ukaguzi uliofanyiwa sajili hiyo ya wapigakura na kampuni ya MPMG. Katika Taarifa Kiongozi wa kampeni za muungano huo Musalia Mudavadi amedai IEBC imekataa kutekeleza mapendekezo yaliyotolewa na KPMG.
Mudavadi amemtaka Mwenyekiti Wafula Chebukati kuelezea mikakati tume hiyo imeweka kuhakikisha watu waliofariki dunia ambao majina yao yangali katika sajili hawatashiriki shughuli ya upigaji kura.
Katika ukaguzi KPMG ilisema kulikuwa na jumla ya majina ya watu elfu mia tisa sabini ya watu waliofariki dunia kati ya mwaka 2012-2016 ambayo yalikuwa katika sajili.?

 

Premium Article

Get Full Access for Ksh299/Week.

Bold Reporting Takes Time, Courage and Investment. Stand With Us.
Continue Reading  →
What you get
  • Unlimited access to all premium content
  • Ad-free browsing experience
  • Mobile-optimised reading
  • Weekly newsletters & digests
Pay via
M - PESA
VISA
Airtel Money
Secure Payments Kenya's most trusted newsroom since 1902
Support Independent Journalism

Stand With Bold Journalism.
Stand With The Standard.

Journalism can't be free because the truth demands investment. At The Standard, we invest time, courage and skills to bring you accurate, factual and impactful stories. Subscribe today and stand with us in the pursuit of credible journalism.

Pay via
M - PESA
VISA
Airtel Money
Secure Payment Kenya's most trusted newsroom since 1902


Related Topics