NA CARREN OMAE
Mhasibu Mkuu wa Serikali Edward Ouko amefika mbele ya Kamati ya fedha ya bunge la Kitaifa kujitetea dhidi ya hoja ya kutaka kumng'atua ofisini. Ouko ameandamana na wakili wake Otiende Omollo, ambaye anatoa maelezo mbele ya kamati kwa niaba ya mhasibu Mkuu huyo.