30th April, 2021
Katibu mkuu wa muungano wa wafanyakazi, Francis Atwoli ameweka historia kama katibu mkuu wa COTU ambaye amehudumu kwa kipindi kirefu. hivi majuzi, atwoli alichaguliwa bila kupingwa kuhudumu kama katibu mkuu wa cotu kwa kipndi cha tano cha miaka mitano. Taifa linapojiandaa kusherehekea sikukuu ya leba dei kesho, mwanahabari wetu mwandamizi patrick amimo alikula ulimi na Francis Atwoli ili kutujuza historia ya muungano wa vyama vya wafanyakazi nchini.