14th January, 2026
Mahakama ya kushughulikia kesi za ugaidi ya Kahawa imewapata na hatia askari watatu wa Gereza la Kamiti kwa kusaidia wafungwa watatu waliokuwa wamehukumiwa kwa makosa ya ugaidi kutoroka kutoka gereza hilo.
Mahakama hiyo iliwapata walinzi Robert Kipkurui Soi, Kaikai Talengo Moses na Willy Wambua na hatia ya kuwezesha kutoroka kwa wafungwa Musharaf Abdala, Mohamed Ali Abikar na Joseph Juma Odhiambo