30th December, 2025
Mwelekeo wa chama cha ODM na mustakabali wa siasa za upinzani nchini huenda ukabadilika, KTN ikibaini kufanyika kwa mikutano ya siri kati ya uongozi wa ODM na chama tawala cha UDA. Inadaiwa kuwa Rais William Ruto alikutana kwa faragha na viongozi wakuu wa ODM katika eneo la Transmara siku ya Krismasi, kwenye mazungumzo ambayo wadadisi wanasema yalilenga kudhoofisha ODM kutoka ndani na hatimaye kuvuta chama hicho kuingia kwenye UDA kabla ya uchaguzi wa 2027. Mwandishi wetu, Herman Kamariki, na taarifa hiyo kwa kina