11th February, 2021
Waakazi wa matunda katika eneo bunge la likuyani walitatiza shughuli za usafiri kwenye barabara ya Eldoret kitale wakidai kuwa afisa mmoja wa polisi katika kituo cha matunda alimlawiti kijana mmoja. Maafisa wa polisi walilazimika kutumia vitoza machozi kuwatawanya wakazi hao ambao walikuwa wameasha moto barabarani. Awali wakazi walikuwa wamekataa kusalimu amri ya polisi ya kuwataka kukoma kuendeleza vitendo vya ghasia