19th October, 2018
Karne moja imepita tangu kuuliwa kwa shujaa Koitalel Arap Samoei ambaye atakumbukwa kwa kuupinga utawala wa mkoloni mweupe. Jamii ya nandi hii leo inaadhimisha miaka mia moja na kumi na mitatu ya kumbukumbu yake. Licha ya Koitalel kuwa shujaa tajika aliyeacha nyayo zake kwenye safu ya mashujaa, kizazi chake kimesahaulika na kusalia kuwa wachochole wanaoishi kwa amri ya mungu.