19th August, 2018
Watu watatu wamepoteza maisha yao katika ajali mbaya ya barabarani iliyotokea katika eneo la Kamureito kwenye barabara ya kutoka mjini Bomet kuelekea Kaplong.
Abiria wengine kumi na tisa walijeruhiwa na kukimbizwa katika hospitali za Kaplong na Tenwek kupokea matibabu.
Taarifa zinasema kuwa matatu hiyo yenye uwezo wa kubeba abiria kumi na nne pekee ilikuwa imebeba jumla ya watu 21 wakati wa ajali hiyo.
Walioshuhudia wanasema kuwa gari hilo lilibingiria mara kadhaa baada ya gurudumu kupasuka.