20th February, 2018
Gavana wa kaunti ya Homa Bay Cyprian Awiti, leo hii amekuwa gavana wa pili kubanduliwa ofisini kufuatia kesi ya uchaguzi. Aliyekuwa mbunge wa Kasipul Kabondo Oyugi magwanga aliwasilisha kesi mahakamani kulalamikia kile alichodai ni kotofuatwa kwa kanuni za uchaguzi na hivyo kupokonywa ushindi.