Mazingira magumu wanayoyapitia wanafunzi wa shule ya msingi ya Nachurur, Pokot Magharibi
17th January, 2016
Je mazingira ya shuleni huathiri matokeo ya wanafunzi masomoni? Bila shaka jibu la swali hilo limo katika shule moja ya msingi katika kaunti ya Pokot Magharibi ambapo wanafunzi hawana vifaa vya masomo yao. Kamche Menza anaangazia mazingira magumu wanayopitia wanafunzi wa shule ya msingi ya Nachurur ambayo pia ina upungufu mkubwa wa walimu.