Mdahalo wa wikendi: Tunaangazia uwezo wa jamii kukuza talanta na kuifanya kitega uchumi
15th March, 2014
Ignatius Juma ni kijana mwenye umri wa miaka 20 ambaye alivuma katika filamu ya “Kibera Kid” iliyoshinda tuzo nyingi kimataifa katika mwaka wa 2006. Wakati huo Ignatius alikuwa na miaka 12 na japo nyota yake ya uigizaji iling’aa wakati huo, Ignatius hajasikika wala kuonekana katika sanaa ya uigizaji tangu wakati huo. Mashirima kapombe alikutana naye Ignatius na kutuandalia taarifa ifuatayo ambayo inahoji uwezo wa jamii kukuza talanta na kuifanya kitega uchumi.