Mpenzi wa mke wa Tuju atiwa nguvuni
31st May, 2013
Mwanamme mmoja anaeyesemekana kuwa na uhusiano wa kimapenzi na mkewe aliyekuwa waziri na mbunge wa Rarieda Raphael Tuju anazuiliwa na polisi kwa kosa la kuingia nyumbani kwa tuju bila ya idhini. Tony Ogunda ambaye na kesi mahakamani inayohusu uhusiano wake na mke wa waziri huyo wa zamani , hata hivyo amemshtaki tuju akidai alipewa kichapo kabla ya kutiwa nguvuni. Tuju na mkewe Rachel wameshafika mahakamani kutaka kutalakiana.