24th December, 2021
Huku sherehe za krismasi zikiendelea kote duniani miongoni mwa wakristo, kinara wa ODM Raila Odinga hii leo aliandaa sherehe kwa watoto mayatima katika boma lake la Riat, kaunti ya Kisumu. Imekuwa desturi yake Odinga kwatembelea marafiki zake na kuandaa sherehe kwake nyumbani pia katika misimu ya krismasi. Kevin Ogutu anatupa picha tofauti ya mwanasiasa Raila Odinga akiwa kwake nyumbani na watoto mayatima.