3rd August, 2021
Kampuni ya Standard imezindua mpango wake wa magazeti katika elimu katika shule ya Mowlem Academy mtaani Umoja hapa jijini Nairobi. Mpango huo unawezesha usambazaji wa gazeti la "The Standard" la kila jumanne, maarufu kama Newspaper In Education (NIE). Tayari shule 258 zimenufaika na mpango huo unaolenga wanafunzi haswa wakati huu mfumo mpya wa umilisi CBC unatekelezwa shuleni.