29th October, 2020
Kamati ya haki na masuala ya sheria katika bunge la seneti tayari limeanza kutathmini mapendekezo ya ripoti ya BBI kabla ya kikao kitakachoandaliwa mjini Naivasha wikendi ijayo kutafuta muafaka.
Spika wa bunge hilo Ken Lusaka amesema kikao hicho, pia kinanuiwa kulinganisha mapendekezo ya bunge hilo kwa jopokazi la BBI yakilinganishwa na ripoti iliyozinduliwa jumatatu.