Jicho Pevu: Kibubusa cha Kanjo (03/04/2016)
3rd April, 2016
Je wajua kuna mtandao mkubwa wa maafisa wa kaunti ya Nairobi unaotumia mbinu kadhaa za hadaa kupata mamilioni ya fedha kinyume cha sheria? Mwanahabari wetu mpekuzi mohamed ali ameyavalia njuga madai ya wachuuzi kwamba ili waruhusiwe kuuza kando kando ya barabara ama hata kwenye masoko ya jijini lazima watoe mlungula wa kila siku kwa watu fulani. Kwenye makala maalum, kibubusa cha kanjo, Mohammed Ali anawafichua maafisa wa kaunti wanaoongoza mtandao huo