Seneta Gedion Moi ataka serikali kutoa hati kwa wakaaji wa Mochongoi
28th June, 2015
Seneta wa baringo gideon moi ameitaka serikali kuharakisha shguli ya utoaji wa hati za umiliki wa mashamba kwa baadhi ya wakaazi eneo la mochongoi. Akizungumza na wakaazi eneo la komoriot mapema hii leo baada ya kuhudhuria ibada katika kanisa la aic komoriot. Gideon alielezea matumaini yake anatarajia serikali itawasilisha hati hizo kabla ya mwisho wa mwaka, ikizingatiwa kuwa wakaazi hao wamekaa bila hati hizo kwa muda wa miaka kumi na miwili wenyeji na viongozi waliokuwepo kwenye mkutano huo walitoa lalama za kukumbwa na ugumu wa kupata mikopo kwa kutumia mashamba waliyokabidhiwa vile vile aliitaka serikali kuwalipa fidia wale waliopoteza makao na mali kutokana na ukosefu wa usalama. Hata hivyo ametoa hakikisho la amani kurejea kufuatia mikakati iliyoafikiwa katika mkutano wa viongozi wa eneo hilo.