×
The Standard Group Plc is a multi-media organization with investments in media platforms spanning newspaper print operations, television, radio broadcasting, digital and online services. The Standard Group is recognized as a leading multi-media house in Kenya with a key influence in matters of national and international interest.
  • Standard Group Plc HQ Office,
  • The Standard Group Center,Mombasa Road.
  • P.O Box 30080-00100,Nairobi, Kenya.
  • Telephone number: 0203222111, 0719012111
  • Email: [email protected]

Watu sita wafarika katika eneo la Sachangwan

News

Watu sita wamefariki dunia na wengine wanane kujeruhiwa baada ya matatu iliyokuwa ikitoka mjini Eldoret kupoteza mwelekeo na kubiringirika kwenye eneo hatari la Sachangwan Barabara Kuu ya Nakuru-Eldoret.

Kamanda wa Polisi wa Molo  Mwenda Muthamia, amesema kuwa wanawake wanne na mwanamume mmoja wamefariki dunia papo hapo huku abiria wengine wanane wakijeruhiwa jana usiku. Majeruhiwa wanatibiwa katika Hospitali ya Molo

Kwingineko,

Watu wawili wamefariki dunia kufuatia ajali iliyohusisha matatu na pikipiki kwenye eneo la Sagana katika Kaunti ya Kirinyaga usiku wa kuamikia leo.

Kamanda wa Polisi wa Kirinyaga Magharibi Wilson Koskei,  amesema kuwa ajali hiyo ilitokea mwendo wa saa moja usiku kwenye Barabara ya Sagana-Karatina.

Koskei amesema kuwa pikipiki hiyo ilikuwa ikielekea upanda wa Sagana kabla ya kupoteza mwelekeo na kugongana na matatu ambapo dereva na mteja wake walifariki dunia katika Hospitali ya Sagana.

Kisa hicho kilisababisha wakazi wenye hamaki kuandamana kutokana na kile wametajwa kuwa usimamizi mbaya wa taasisi hiyo.

Wakiongozwa na Peter Ndirangu wamelalamikia ukosefu wa huduma bora na dawa katika hosputlia hiyo. Aidha wanataka Barabara ya Sagana-Karatina kuwekwa matatu ili kuzuia ajali za mara kwa mara.

Related Topics


.

Trending Now

.

Popular this week