Chama cha Kitaifa cha Walimu wa Shule za Upili na Vyuo vya Kadri KUPPET kimezitetea baadhi ya shule ambazo matokeo yake ya mitihani ya Kitaifa ya Kidato cha Nne mwaka jana, yaliimarika pakubwa kulinganishwa na awali.
Katibu Mkuu wa Chama hicho Akello Misori, amesema kuna uwezekano mkubwa kwa matokeo ya watahiniwa kutofautiana kila mwaka kutokana na sababu mbalimbali; mfano kuimarisha hali ya masomo na hata kubadilishwa kwa walimu na wakati mwingine watahiniwa kuwa werevu kulinganishwa na watangulizi wao.