×
App Icon
The Standard e-Paper
Kenya’s Boldest Voice
★★★★ - on Play Store
Download App

Amin Mohamed Ibrahim ndiye Mkurugenzi mpya wa Idara ya Upelelezi DCI

Amin Mohamed Ibrahim ndiye Mkurugenzi mpya wa Idara ya Upelelezi, DCI baada ya kuteuliwa rasmi na Rais William Ruto. Uteuzi wa Amin umechapishwa katika Gazeti Rasmi la Serikali. Kabla ya uteuzi wake, Amin alikuwa Mkuu wa Kitengo cha Usimamizi wa masuala ya Ndani katika Idara ya Polisi internal Affairs Unit IAU.

Kabla ya hapo alikuwa msimamizi wa kitengo cha uchunguzi katika makao makuu ya DCI. Amewahi kuhudumu katika vitengo vingine mbalimbali kama kile cha upelelezi wa uhalifu wa kifedha .

Alipandishwa cheo na kuwa Naibu Inspekta Mkuu wa Polisi Mwezi Machi mwaka jana. Uteuzi wa Amin umefanyika baada ya jumla ya watu kumi waliorodheshwa kwa mchujo kuhojiwa wiki iliyopita. Waliohojiwa ni Bernard Barasa Walumoli, Eliud Kipkoech Lagat, Gideon Nyale Munga, Esther Chepkosgei Seroney na David Kipkosgey Birech. Wengine ni Jonyo Michael Wiso, Nicholas Ireri Kamwende, Paul Jimmie Ndambuki na Simon Mwangi Wanderi.

Get Full Access for Ksh299/Week
Fact‑first reporting that puts you at the heart of the newsroom. Subscribe for full access.
  • Unlimited access to all premium content
  • Uninterrupted ad-free browsing experience
  • Mobile-optimized reading experience
  • Weekly Newsletters
  • MPesa, Airtel Money and Cards accepted
Already a subscriber? Log in