Muungano wa Wafanyakazi wa Hoteli, Taasisi za Elimu na Hospitali, KUDHEIHA umetoa notisi ya mgomo ya siku 14 kwa usimamizi wa Chuo Kikuu cha Egerton kutekelezwa kwa mkataba wa makubaliano baina yao.
Katibu Mkuu wa Chama hicho Albert Njeru ameulamu usimamizi kwa kushindwa kuwalipa wafanyakazi.
Muungano huo sasa unataka chuo hicho kutekeleza makubaliano hayo la sivyo wagome kufikia tarehe 31 mwezi huu.
Haya yanajiri huku Muungano wa Wafanyakazi wa Vyuo Vikuu UASU ukitoa notisi kwa Chuo hicho cha Egerton kuanza kuwapa wafanyakazi wake mishahara yote lasi sivyo wagome kufikia mwisho wa mwezi huo.
Chuo hicho kimekukuwa kikikumbwa na changamoto za kifedha huku ikidaiowa mamilioni ya fedha na hata kusababishwa kufungwa kwake mara kadhaa.