×
The Standard Group Plc is a multi-media organization with investments in media platforms spanning newspaper print operations, television, radio broadcasting, digital and online services. The Standard Group is recognized as a leading multi-media house in Kenya with a key influence in matters of national and international interest.
  • Standard Group Plc HQ Office,
  • The Standard Group Center,Mombasa Road.
  • P.O Box 30080-00100,Nairobi, Kenya.
  • Telephone number: 0203222111, 0719012111
  • Email: [email protected]

Magoha asisitiza kuwa shule zitafunguliwa Alhamisi

News

Waziri wa Elimu Profesa George Magoha amesema tarehe ya kurejelewa rasmi kwa shughuli za elimu nchini baada ya kipindi cha wiki mbili itasalia jinsi ilivyo yaani kesho Alhamisi tarehe 18.

Shule zilifungwa kwa wiki mbili kupisha maandalizi ya uchaguzi uliofanyika tarehe tisa mwezi huu.

Akizungumza katika Shule ya Upili ya Mwangaza jijini Nairobi wakati wa uzinduzi wa madarasa ya kufanikisha Mtalaa wa Umilisi, CBC Magoha ametetea hatamu yake ya uongozi akisema ameafikia malengo yaliyowekwa na serikali kuhusu sekta ya elimu.

Magoha ameendelea kuwaomba Wakenya msamaha kutokana na kauli zake anazosema zilifasiriwa visivyo akisisitiza kuwa lengo lake ni kuinua sekta ya elimu.

Licha ya changamoto mbalimbali wakati wa hatamu yake mfano athari za janga la korona katika sekta ya elimu, Magoha amesema ametekeleza wajibu wake ifaavyo.

Waziri amejibu swali la wanahabari kuhusu uwezekano wa kuathiriwa tena kwa kalenda ya elimu akisema mikakati imewekwa kuzuia kusitisha masomo endapo patakuwa na chaguzi nyingine mfano kuhamishwa kwa vituo vya kupigia kura vilivyowekwa shuleni hadi maeneo mengine.

Kufikia sasa, ujenzi wa madarasa hayo ya CBC umefikia asilimia 75 kote nchini huku Kauti ya Nyeri ikiwa tayari imefanikisha ujenzi wa asilimia mia moja. Jumla ya madarasa 6,500 yamekamilisha na kusalia 1,200.

Kaunti za maeneo ya Kati na Nyanza zimeafikia ujenzi wa asilimia 90 huku Kaskazini na Mashariki yakiwa na asimia ndogo ya ujenzi huo.

Haya yanajiri huku Wizara ya Elimu ikiwa imefungua wavuti wake kwa umma kufanikisha shughuli za usajili wa wanafunzi watakaojiunga na Shule za Upili Daraja ya Chini, yaani Junior Secondaary.

Related Topics


.

Trending Now

.

Popular this week