×
The Standard Group Plc is a multi-media organization with investments in media platforms spanning newspaper print operations, television, radio broadcasting, digital and online services. The Standard Group is recognized as a leading multi-media house in Kenya with a key influence in matters of national and international interest.
  • Standard Group Plc HQ Office,
  • The Standard Group Center,Mombasa Road.
  • P.O Box 30080-00100,Nairobi, Kenya.
  • Telephone number: 0203222111, 0719012111
  • Email: [email protected]
Premium

Rais Kenyatta azindua rasmi Nairobi Expressway

News

Rais, Uhuru Kenyatta hatimaye amezindua rasmi matumizi ya barabara ya mwendo-kasi ya Nairobi Express Way baada ya ujenzi wake kukamilika.

Akizungumza wakati wa shughuli ya uzinduzi huo, Rais amesema kwamba chini ya uongozi wake Kenya imepiga hatua kubwa katika kuimarisha muundo msingi.

Aidha amesema Barabara ya Expressway imechangia pakubwa katika kupunguza msongamano wa magari hasa katika Barabara Kuu ya Nairobi-Mombasa, kupunguza gharama ya uchukuzi kando na kubuni nafasi za kazi.

Barabara hiyo ya umbali wa kilomita 27, inayoanzia Mlolongo hadi barabara ya James Gichuru katika Mtaa wa Westlands, ilijengwa na kampuni ya China Road and Bridge Corporation.Barabara hiyo ilifungwa jana usiku kwa muda baada ya kipindi cha majaribio kukamilika kabla ya kuzinduliwa rasmi leo hii.Kampuni Moja Expressway imekuwa ikisimamia mchakato huo wa majaribio kuanzia mwezi Mei mwaka huu wa 2022.

Awali, Rais Kenyatta alizindua rasmi barabara ya pembezoni ya mashariki ikiwa na safu nne hadi sita.Barabara hiyo itahudumia wakaazi wa eno la Njiru na Ruai kwa kumaliza msongamano na kufungua nafasi za ajira na biashara.

Related Topics


.

Trending Now

.

Popular this week